Kiswahili
Azimio La Nambari 275 (Azimio 275) La Tume Ya Haki Za Binadamu Na Za Watu Ya Afrika
Utangulizi
Azimio la nambari 275 (Azimio 275) la Tume ya Haki za Binadamu na za Watu ya Afrika, ” Ulinzi Dhidi ya Unyanyasaji na Ukiukaji wa Haki za Binadamu dhidi ya Watu kwa Msingi wa Hisia au Jinsia ” lilipitishwa mnamo 2014. Azimio hilo linalaani dhulma kwa msingi wa wa hisia halisi au zinazodhaniwa na mwelekeo wa kijinsia. Azimio 275 linashauri nchi za Kiafrika, watendaji wa serikali na wasio wa serikali; kuzuia, kuchunguza, na kurekebisha vitendo vya ukatili vinavyotokana na dhulma kwa msingi wa hisia halisi au inayodhaniwa na mwelekeo wa kijinsia.
Tume ya Haki za Binadamu na za Watu ya Afrika ni chombo huru kilichoanzishwa na Hati ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika (Hati ya Banjul) kukuza na kulinda haki za binadamu za kila mtu barani Afrika. Azimio 275 ni maandishi ya kwanza ya kisheria juu ya ukiukaji na dhuluma kwa msingi wa hisia na jinsia uliyopitishwa na tume hii.
Nakala ya Azimio 275
275: ” Ulinzi Dhidi ya Unyanyasaji na Ukiukaji wa Haki za Binadamu dhidi ya Watu kwa Msingi wa Hisia au Jinsia “
Tume Ya Haki Za Binadamu Na Za Watu Ya Afrika Katika Mkutano Wake Wa 55 Wa Kawaida Uliofanyika Luanda, Angola, Kutoka Aprili 28 – Mei 12 2014:
Kumbuka kwamba Kifungu cha 2 cha Hati ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika (Hati ya Banjul) kinakataza ubaguzi wa mtu yoyote kwa misingi ya tofauti za aina yoyote kama kabila, rangi, jinsia, lugha, dini, maoni ya kisiasa, asili ya kitaifa au kijamii, bahati, kuzaliwa au hali yoyote;
Kwa kukumbuka zaidi kwamba Kifungu cha 3 cha Hati ya Bajul kinampa kila mtu kinga sawa ya kisheria;
Kwa kuzingatia kwamba Kifungu cha 4 na 5 cha Hati ya Banjul kinawapa kila mtu heshima ya maisha yao na uadilifu wao, na kuzuia kuteswa na unyanyasaji mwingine mbaya, wa kinyama na udhalilishaji au kuteswa;
Tunashituka kwamba vitendo vya dhuluma, ubaguzi na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu unaendelea kufanywa kwa watu katika sehemu nyingi za Afrika kwa sababu ya hisia yao halisia ya kimapenzi au ya kudhaniwa au mwelekeo wao wa kijinsia;
Tumegundua kuwa unyanyasaji kama huu ni pamoja na ubakaji, kushambuliwa kimwili, kuteswa, mauaji, kukamatwa kwa kiholela, kufunguliwa mashtaka, kupotezwa kwa nguvu, unyang’anyi na jinai;
Zaidi ya hayo tuna wasiwasi kwamba matukio haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu pia yanalenga watetezi wa haki za binadamu na mashirika yanoyofanya kazi dhidi ya kuangamiza ubaguzi, dhulma na unyanyasaji wa mtu yoyote kwa ajili ya hisia au jinsia yake.
Tunasikitishwa sana na uzembe wa vyombo vya kutekeleza sheria kufanya uchunguzi wa kina na kuwashtaki wahusika wa dhulma na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu unaolenga watu kwa misingi ya hisia au jinsia:
- Tunalaani kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu, mauaji, ubakaji, kushambulia, kufungwa jela na aina nyingine za udhalilishaji wa watu kwa msingi wa hisia na jinsia.
- Hususan tunalaani mashambulio ya kimfumo yanayotekelezwa na watendaji wa kiserakali na wasio wa serikali dhidi ya watu kwa misingi ya hisia na jinsia.
- Wito kwa Mataifa kuhakikisha kuwa watetezi wa haki za binadamu wanafanya kazi katika mazingira yanayowawezesha kutokuwa na unyanyapaa, kulipiza kisasi au mashtaka ya jinai kwa sababu ya shughuli zao za kutetea haki za binadamu, pamoja na haki za watu wanaodhulumiwa kwa ajili ya hisia zao za kimapenzi; na
- Tunahimiza sana Mataifa kumaliza vitendo vyote vya dhuluma na unyanyasaji, vinanyotekelezwa na wahusika wakiserekali au wasio wa serikali, pamoja na kutunga na kutekeleza sheria zinazofaa, zinazokataza na kuadhibu aina zote za dhuluma kwa misingi ya hisia na jinsia, kuhakikisha uchunguzi sahihi na mashtaka ya wahalifu, na kuanzisha taratibu za mahakama zinazojibu mahitaji ya wahasiriwa.
Lilopitishwa katika Mkutano wa 55 wa Kawaida wa Tume Ya Haki Za Binadamu Na Za Watu Ya Afrika Nchini Luanda, Angola, Aprili 28 – Mei 12, 2014